AIIB yazindua mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2023-09-26 09:15:21| CRI

Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) imezindua Mpango wa Utekelezaji wa Juhudi za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (CAP), ambao unatajwa kama hatua muhimu ya kutimiza ahadi yake katika kukabiliana na changamoto hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo inasema mpango huo unatarajiwa kuelekeza juhudi zake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kati ya mwaka 2024 hadi 2030, na umeunganisha kanuni za usimamizi wa kukusanya fedha, na kubainisha sekta muhimu ambazo itatumia uwekezaji wake kusaidia nchi wanachama wake.

Mkuu wa AIIB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw. Jin Liqun amesema, mpango huo umedhihirisha nia ya Benki hiyo ya kukusanya mitaji, uwezo, na ushawishi ili kuzisaidia nchi wanachama kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.