Kenya yatoa dola milioni 2.3 za kimarekani kwa kaya katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame
2023-09-26 09:17:15| CRI

Kenya imetangaza kuwa imetoa dola milioni 2.3 za kimarekani chini ya mradi wa usalama na kukabiliana na njaa (HSNP), ili kuokoa kaya katika maeneo yanayoathiriwa na ukame nchini humo. 

Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ardhi kame na nusu kame ASAL na maendeleo ya mikoa Bibi Rebecca Miano, amesema kaya laki 1.19  zenye mahitaji na hali duni katika kaunti za Marsabit, Wajir, Mandera Turkana, Samburu, Isiolo, Garissa na mto wa Tana zitanufanika na msaada huo wa kifedha. 

Bibi Miano ametoa taarifa huko Nairobi akisema, kaunti zilizotajwa ni kati zile zinazoathiriwa vibaya zaidi na ukame unaodumu kwa misimu minne ya mvua. 

Kwa mujibu wa mamlaka ya taifa ya usimamizi wa ukame, mwezi wa Agosti idadi ya wakenya wenye mahitaji ya msaada wa chakula ilifikia milioni 2.8 katika kaunti 23.