Barabara ya Kenya iliyojengwa na China yatunukiwa tuzo ya kikanda
2023-09-26 09:12:01| CRI

Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi iliyojengwa na China nchini Kenya imepewa tuzo ya “uvumbuzi bora wa teknolojia katika sekta ya usafiri” kwenye awamu ya pili ya Tuzo ya Afrika Mashariki.

Kampuni iliyoendesha ujenzi wa barabara hiyo imepewa tuzo hiyo kutokana na mfumo wake wa ulipaji wa pesa wa elektroniki (ETC), ambao ni uvumbuzi unaoruhusu waendesha magari kulipa kwa urahisi wanapotumia barabara hiyo.

Ili kuwezesha huduma hiyo, mtu anayejiandikisha kwa kutoa nakala ya kitambulisho chao na kitabu cha kumbukumbu, na magari yao yanawekwa chip ambayo itawawezesha watu kulipia huduma hiyo kwa kuingiza pesa. Mfumo wa ETC unavutia waendesha magari kwani unaokoa muda.