Waziri Mkuu wa Canada ajutia kupongezwa bungeni kwa mtu aliyepigania wanazi
2023-09-26 09:14:52| CRI

Waziri Mkuu wa Canada Bwana Justin Trudeau amelaani bunge la Canada kumpongeza kwa bahati mbaya mwanajeshi mkongwe aliyepigania uhuru wa Ukraine kwa niaba ya wanazi wakati wa vita ya pili ya Dunia.

Akiongea na wanahabari kwenye bunge la Canada Bwana Trudeau amelitaja tukio hilo kama la "kusikitisha sana", na kusema spika wa Bunge amekiri makosa yake na ameomba msamaha. Amesema tukio hili sio la kusikitisha kwa bunge la Canada peke yake, bali ni kwa wacanada wote.

Bwana Trudeau amesema hayo baada ya kujulikana kuwa wabunge wa Kanada walionyesha heshima kwa Yaroslav Hunka raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 98, muda mfupi baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhutubia bunge kama sehemu ya ziara yake nchini humo, lakini siku mbili baadaye ilijulikana kuwa mtu huyo alikuwa sehemu ya kitengo cha wanazi kinachopigania uhuru wa Ukraine.