Wadhibiti wa viwango wa Afrika wakutana kuimarisha biashara ya kuvuka mpaka
2023-09-26 09:14:35| CRI

Wadhibiti wa viwango wa nchi za Afrika wameanza mkutano wa siku tano huko Nairobi, kujadili njia za kuimarisha biashara ya kuvuka mpaka kupitia uratibu wa vigezo vya bidhaa zinazozalishwa barani humo.

Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 100 kutoka mamlaka za udhibiti wa viwango za nchi za Afrika, ili kutafuta utambuzi wa pamoja wa vigezo vya bidhaa barani Afrika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda ya Kenya Bw. Juma Mukhwana, amesema kuwepo kwa vigezo tofauti vya bidhaa barani Afrika ni moja ya vizuizi vikuu kwa biashara kati ya nchi za Afrika, na mfumo wa pamoja wa vigezo vya bidhaa utaongeza imani kwa bidhaa zinazotengenezwa barani Afrika, na si kama tu utahimiza biashara ya ndani, bali pia utahimiza biashara ya bara zima.