Jeshi la Sudan na vikosi vya kijeshi vyapambana vikali karibu na makao makuu ya jeshi
2023-09-26 09:12:32| CRI

Mashuhuda wamesema Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimepambana karibu na makao makuu ya jeshi.

Kundi la RSF lilifanya mashambulizi dhidi ya makao makuu ya jeshi kutoka kambi zake kusini mwa Khartoum.

Katika siku 10 zilizopita RSF imekuwa ikifanya mashambulizi ya makombora dhidi ya vikosi vya jeshi. SAF imejibu mashambulizi makali ya silaha katika vitongoji kadhaa kwenye eneo la mashariki mwa Nile, katika mji wa Bahri.

Wakati huo huo, chumba cha utoaji wa huduma za dharura kilichoko kwenye wilaya ya Al-Jarif Sharq, kitongoji cha kaskazini mwa Khartoum, kimesema katika taarifa yake kuwa eneo hilo limeshambuliwa vibaya, na kuwataka wakazi kubaki ndani ya nyumba zao na kukaa mbali na milango na madirisha.