China na Zimbabwe zatakiwa kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari ili kukabiliana na umwamba wa habari wa nchi za Magharibi
2023-09-26 10:11:06| CRI


Mtaalamu wa Uhusiano kati ya Zimbabwe na China, ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari nchini Zimbabwe Bw. Tichaona Zindoga amesema ni muhimu kwa China na Zimbabwe kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari ili kukabiliana na umwamba wa habari wa nchi za magharibi.

Bw. Zindoga amesema hayo alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) ambapo amesema, Zimbabwe na China zimekuwa na ushirikiano katika sekta ya vyombo vya habari kwa miaka mingi, na njia ya uendeshaji wa vyombo vikubwa vya habari ya China na matumizi ya teknolojia ya kisasa zinachangia maendeleo ya vyombo vya habari nchini Zimbabwe.

Pia amesema, taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi dhidi ya nchi zinazoendelea duniani zikiwemo China na Zimbabwe ni umwamba wa habari. Amesema China na Afrika zinatakiwa kuimarisha ushirikiano wa karibu katika habari na mawasiliano ya vyombo vya habari ili kuchukua nafasi ya thamani ya maadili inayoshikiliwa na nchi za magharibi.