Wamiliki wa meli Zanzibar waingiwa na wasiwasi wakati AGL ikichukua mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bandari ya Malindi
2023-09-26 14:41:35| cri

Wamiliki wa meli Zanzibar wamelalamikia mabadiliko ya taratibu na gharama baada ya serikali kukabidhi mamlaka ya usimamizi wa shughuli za Bandari ya Malindi kwa kampuni ya Ufaransa.

Jumatatu, Shirika la Bandari Zanzibar lilikabidhi mamlaka ya usimamizi wa bandari hiyo kwa Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL), huku ikitarajia kuongezeka kwa ufanisi na mapato ya bandari hiyo.

Siku chache baada ya kuchukua mamlaka, wamiliki wa meli walilalamikia kubadilishiwa taratibu za kutia nanga na malipo, hatua ambayo wanasema itaongeza gharama za uagizaji.

Waendeshaji wa Majahazi walilalamika kuwa ada zimeongezeka karibu maradufu tangu mwendeshaji mpya wa bandari kuanza kufanya kazi.

Hata hivyo maafisa wa serikali walitetea ada hizo mpya wakisema ziliwekwa tangu mwaka 2018 lakini zilikuwa bado hazijatekelezwa.