Tamasha la Filamu za Documentary za China lafanyika Chile
2023-09-26 15:31:26| cri

Kabla ya kutimia miaka 10 ya kutolewa kwa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG likishirikiana na Tume ya Uchumi ya Amerika ya Kusini ya Umoja wa Mataifa wamefanya Tamasha la Filamu za Documentary za China kuhusu jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na Ukanda Mmoja, Njia Moja mjini San Diego, makao makuu ya Tume hiyo nchini Chile.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong amesema katika miaka kumi iliyopita, pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limeshikilia kanuni za kushauriana, kujenga na kunufaika kwa pamoja, na kuhimiza kukamilika kwa miradi mbalimbali halisi katika sekta za biashara, viwanda na utamaduni na kunufaisha watu wa nchi mbalimbali.