Kenya yachapisha kitabu cha kwanza cha kufundisha lugha ya kichina kinacholingana na hali halisi ya Afrika Mashariki
2023-09-27 08:46:14| CRI

Hafla ya utiaji saini Uchapishaji wa Kitabu cha Mafunzo ya Lugha ya Kichina kwa ajili ya Afrika Mashariki imefanyika jana katika Taasisi cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Hiki ni kitabu cha kwanza cha kufundisha kichina kulingana na umaalumu wa mafundisho ya lugha ya kichina katika eneo la Afrika Mashariki.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi Professor Stephen Kiama Gitahi amesema uchapishaji wa kitabu hicho utachangia kuboresha kazi ya ufundishji ya walimu barani Afrika, na kuwawezesha wanafunzi na walimu wa Afrika kupata uzoefu zaidi kuhusu mvuto wa utamaduni wa China.

Mwalimu wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi Liang Yu, amesema kitabu hiki kilitungwa kwa kufuata vigezo vya lugha ya kichina vilivyotangazwa mwaka 2021, na kinafaa zaidi kwa wanafunzi wa lugha ya kichina kupitia mitihani ya kupima ustadi wa lugha ya kichina.