Sudan Kusini yapongeza uhusiano na China
2023-09-27 08:58:16| CRI


 

Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umefanya hafla ya kusherehekea miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC) .

Kwenye hafla hiyo Waziri wa Mambo ya Ikulu ya Sudan Kusini Bw. Barnaba Marial Benjamin, ametoa wito wa kujenga jumuiya ya kimataifa yenye hatma ya pamoja, na kusisitiza kwamba dunia inahitaji zaidi ushirikiano wa pande zote kuliko zamani, ili kuendeleza maendeleo ya binadamu wote.

Amesema mambo yaliyofanywa na China nchini Sudan Kusini katika muda wa mpito tangu Sudan Kusini kupate uhuru yanafurahisha, zaidi ya kutoa msaada China pia imeingia katika nyanja ya maendeleo, hali ambayo itaboresha maisha ya watu wa Sudan Kusini.  

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Ma Qiang amesema, uaminifu wa kisiasa kati ya China na Sudan Kusini umeimarishwa, na China daima inaheshimu mamlaka na uhuru wa Sudan Kusini, na kupinga kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya Sudan Kusini. Ameongeza kuwa China imetoa sauti kwa ajili ya maslahi ya Sudan Kusini katika majukwaa ya pande nyingi ikiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono mchakato wa amani nchini humo kwa hatua halisi.