Ubalozi wa China watoa tuzo za shindano la upigaji picha na video za maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya China na Kenya
2023-09-27 08:48:46| CRI

Ubalozi wa China nchini Kenya umeandaa hafla ya kutoa tuzo kwa baadhi ya wakenya na wachina walioshiriki kwenye mashindano ya upigaji picha yenye mada ya“mustakabali wa pamoja”, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya China na Kenya, sambamba na maadhimisho ya miaka 10 yangu pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja. Picha hizo zinahusu mambo mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Kenya kama vile miundombinu na mabadilishano ya watu kwa watu. Hafla hiyo imeandaliwa na taasisi ya Confucius katika chuo kikuu cha Nairobi.