Rais Xi Jinping asisitiza ujenzi wa maeneo ya biashara huria ya kiwango cha juu
2023-09-27 08:47:55| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza juhudi za kujenga maeneo ya majaribio ya biashara huria ya ngazi ya juu (FTZs), na kutaka maeneo hayo kuwa nafasi ya mbele na kukabiliana na changamoto ngumu.

Rais Xi amesema kwenye maagizo aliyotoa hivi karibuni kuhusu kuendeleza maeneo ya biashara huria, akisema ujenzi wa maeneo hayo umekuwa ni hatua muhimu ya kimkakati ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika kuhimiza mageuzi na ufunguaji mlango katika zama mpya.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, maeneo ya biashara huria yametumika kama mbinu ya kina ya majaribio kwa ajili ya mageuzi na ufunguaji mlango, kwa kuleta sera nyingi mpya na kuwa na matokeo mengi ya kihistoria.