Mjukuu wa Nelson Mandela Zoleka afariki dunia kwa saratani akiwa na umri wa miaka 43
2023-09-27 23:18:21| cri

Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Nelson Mandela, Zoleka Mandela, amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 43.

Akitangaza kifo chake siku ya Jumanne, msemaji wa familia alisema Zoleka ambaye ni mwandishi aliyejulikana kwa kuelezea vita vyake vya muda mrefu dhidi ya ugonjwa huo, alilazwa hospitalini Jumatatu kama sehemu ya matibabu yake yanayoendelea.

Alikuwa mtoto wa binti mdogo wa Mandela, Zindzi Mandela, na mume wake wa kwanza, Zwelibanzi Hlongwane. Familia hiyo ilisema uchunguzi wa hivi karibuni ulionesha saratani yake ambayo iliathiri nyonga, ini, mapafu, pelvis, ubongo na uti wa mgongo, ilikuwa imeenea zaidi.