Zanzibar na taasisi za China wasaini makubaliano ya ushirikiano
2023-09-27 14:22:01| cri

Taasisi kadhaa kutoka China, zikiwemo Mji wa Weihai na mkoa wa Shandong, zimesaini Makubaliano ya Maelewano (MoU) na Zanzibar na baadhi ya wizara za Visiwani humo kwa ajili ya kujenga uwezo, biashara na maeneo mengine ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga, baada ya utiaji saini huo uliofanyika Zanzibar.

Akikaribisha makampuni kutoka China na sehemu nyingine za Dunia alisema Zanzibar imekuwa ikichukua hatua tofauti za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Pamoja na mikataba mingine, Makubaliano yaliyosainiwa kati ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar na Ofisi ya Biashara ya Wilaya ya Weihai Wendeng ya China, yanalenga kuweka mfumo wa ushirikiano wa kukuza na kuwezesha shughuli za biashara na uchumi kati ya mkoa wa Shandong wa China na Zanzibar. pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Makubaliano mengine yaliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Shirika la CNTIC-MEHECO la China yalikuwa ya ‘mradi wa kuboresha uwezo wa huduma ya afya ya msingi wa kidijitali.