Tanzania yakaribisha wawekezaji zaidi kutoka China kuunga mkono maendeleo ya viwanda
2023-09-27 09:03:13| CRI

Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema serikali ya Tanzania imefungua milango yake kwa wawekezaji zaidi ili kuunga mkono msukumo wa ujenzi wa nchi hiyo.

Bw. Majaliwa amewahakikishia wawekezaji wa China kwamba Tanzania iko tayari kufanya biashara na wawekezaji wa China na milango iko wazi, wakati akifunga mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Zhejiang (Jinhua) na Tanzania wa jukwaa la uwekezaji kati ya China na Tanzania uliofanyika huko Dar es Salaam.

Amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya biashara, sera nzuri za kiuchumi, utulivu wa ujumla wa uchumi, maliasili nyingi, nguvukazi iliyoelimika na soko kubwa kwa sababu ya eneo la kipekee la kijiografia la nchi.

Jukwaa hilo limewavutia wajumbe zaidi ya mia moja wa kiuchumi na kibiashara walioongozwa na kamati ya mkoa wa Zhejiang ya baraza la kuhimiza biashara za kimataifa la China (CCPIT) na serikali ya mji wa Jinhua ya mkoa wa Zhejiang, China.