Katibu Mkuu wa CPC asisitiza ushiriki katika mageuzi ya WTO
2023-09-28 14:11:29| cri

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping, amesisitiza juhudi zaidi ili kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kuboresha uwezo wa kushughulikia ufunguaji mlango wa ngazi ya juu.

Xi amesema hayo alipoongoza kikao cha kikundi cha mafunzo cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC kilichofanyika jana mjini Beijing. Amesema ni mwafaka wa pamoja na mwelekeo wa kawaida wa kutekeleza mageuzi yanayohitajika ya Shirika hilo, kutokana na kwamba WTO ni nguzo muhimu ya pande nyingi na ngazi muhimu kwa usimamizi wa uchumi wa dunia.

Pia Bw. Xi ametoa wito wa kulinda kithabiti mamlaka na ufanisi wa utaratibu wa biashara ya pande nyingi huku WTO ikiwa ni msingi mkuu, na kuhimiza kihalisi kurejeshwa kwa uendeshaji wa kawaida wa mfumo wa kusuluhisha migogoro wa Shirika hilo.