Kenya yajitahidi kupanua mipango ya nishati safi
2023-09-28 09:11:39| CRI


 

Wanaviwanda wa Kenya wameahidi kupanua mipango yao ya kuendeleza nishati safi, ili nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuwa na mustakabali wa kutoa kaboni dioksidi chache.

Kwenye Maonesho ya 9 ya Nishati Safi yaliyofanyika huko Nairobi, mtendaji mkuu wa Shirikisho la Utengenezaji la Kenya Bw. Anthony Mwangi, amesema sekta ya uzalishaji viwandani ya Kenya imeanzisha mipango kadhaa ambayo itaongeza matumizi ya nishati mbadala ikiwemo upepo, maji na jua katika shughuli zake.

Maonesho hayo yameshirikisha zaidi ya wajumbe 100 wakiwemo maafisa waandamizi wa serikali na wataalam wa nishati, na yameonesha matokeo ya uvumbuzi katika sekta ya nishati safi, ikiwemo nishati mbadala, maji, magari ya kielektroniki, ujenzi wa kijani, na upishi kwa njia safi.