Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana ilifanya mkutano, kwa lengo la kukagua na kujadili ripoti ya ukaguzi wa nidhamu.
Mkutano huo umesema, Kamati Kuu ya CPC na Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Bw. Xi Jinping inatilia maanani sana ukaguzi wa nidhamu, kufanya maamuzi mfululizo na kuweka mipango muhimu.
Mkutano huo pia umesema, ukaguzi wa nidhamu ni njia yenye ufanisi ya kutambua na kutatua masuala, na unapaswa kuendelea kutekelezwa.