Waziri wa Ghana apongeza ushirikian na China
2023-09-28 09:11:02| CRI


 

Waziri wa Fedha wa Ghana Bw. Kenneth Ofori-Atta amesema ushirikiano kati ya Ghana na China umekuwa nguzo ya maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Akihutubia hafla ya kuadhimisha miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Ofori-Atta ameishukuru China kwa kuunga mkono Ghana katika sekta zote za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuisaidia nchi hiyo kupata mkopo wa dola bilioni 3 za kimarekani kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. Ameongeza kuwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili umeinufaisha Ghana katika sekta za miundombinu, elimu, ulinzi, kilimo, upashanaji habari na uvuvi.

Naye balozi wa China nchini Ghana Bw. Lu Kun amesema katika miongo kadhaa iliyopita, ushirikiano kati ya China na Ghana umekuwa na mafanikio, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa Ghana.