Rais wa Jamhuri ya Kongo atumai kuinua ngazi ya uhusiano kati ya nchi yake na China
2023-09-28 08:58:50| CRI

Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo amesema, Kongo na China ni marafiki, wenzi na ndugu, na anapenda kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati na ushirikiano wa pande zote kati ya nchi mbili katika kiwango cha juu zaidi.

Rais Nguesso amesema hayo wakati akipokea hati ya utambulisho ya balozi wa China nchini humo Bw. Li Yan. Amesema ana matarajio makubwa na maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi mbili yatakayofanyika mwaka kesho, na kutaka kutumia fursa hiyo kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi mbili.

Bw. Li amesema chini ya uongozi wa viongozi wa nchi mbili, uhusiano wa wenzi wa kimkakati na ushirikiano wa pande zote kati ya Kongo na China unaendelea kuimarika, na katika muda wake wa kazi, anapenda kushirikiana na upande wa Kongo kutimiza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi mbili.