Japan kumwaga maji taka ya nyukilia baharini kwasababisha hasira kubwa ya jamii ya kimataifa
2023-09-28 14:18:40| CRI

Kampuni ya Umeme ya Tokyo ya Japan imetangaza kuwa imemaliza awamu ya kwanza ya kumwaga maji taka ya nyuklia baharini, na awamu ya pili inatarajiwa kuanza hivi karibuni. Tangu Japan ilipoanza kumwaga maji taka ya nyukilia baharini, kitendo hiki kimesababisha hasira kubwa ya jamii ya kimataifa.  

Mwaka 2011, tetemeko kubwa la ardhi na tsunami iliyotokana na tetemiko hilo vilisababisha uvujaji wa nyuklia kwenye Kiwanda cha Umeme cha Nyuklia cha Fukushima nchini Japana. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ambayo inamiliki kiwanda hicho, imehifadhi mamilioni ya tani za maji yenye mionzi yanayotumiwa kupoza mitambo ya nyukilia. Mwaka 2021, serikali ya Japan ilitangaza kwamba itamwaga maji hayo baharini, ikidai kuwa maji hayo hayataleta athari kwa baharini.

Hata hivyo, hadi sasa Japan imeshindwa kuthibitisha kuwa maji hayo ni salama kwa mazingira ya bahari. Wataalamu wa nyuklia wa Greenpeace wanasema, kaboni iliyo katika maji taka ya nyuklia ya Japan ina hatari itakayoendelea kwa maelfu ya miaka, na inaweza kusababisha uharibifu wa jeni ya viumbe.

Japan kumwaga taka za nyuklia baharini kwanza kumesababisha hasira ya raia wake wenyewe. Watu wengi wamefanya maandamano mbele ya Ikulu na idara husika za serikali, wakitaka kuacha mara moja kitendo hicho cha kuchafua bahari. Watu kutoka Fukushima na maeneo ya jirani wamesema kitendo hicho hakivumiliki kabisa, na serikali imepuuza upinzani mkali wa wavuvi wa Fukushima na wananchi wake. Shirikisho la Watu Wanaopinga Kumwaga Maji Taka ya Nyukilia Baharini limewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya rais Fumio Kishida, na Kiongozi wa Kampuni ya Umeme ya Tokyo ya Japan Tomaki Kobayakawa, kwa tuhuma za vifo vinavyotokana na uzembe.

Mpango huu wa Japan pia umepingwa vikali na nchi jirani zake. China imeilaumu Japan kwa kupuuza wasiwasi na upinzani wa jumuiya ya kimataifa na kumwaga maji taka ya nyuklia kwenye Bahari ya Pasifiki kama “mfereji wa maji taka”. Mjumbe wa kudumu wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa Kim Sung hivi karibuni amelaani serikali ya Japan na kusema kitendo hicho kitaleta madhara yasiyoweza kurekebishwa kwa usalama wa binadamu na mazingira ya baharini. Korea Kusini iko karibu sana na Japan. Baada ya Japan kuanza majaribio ya kumwaga maji taka ya nyuklia, watu wa Korea Kusini walinunua chumvi nyingi, wakiwa na wasiwasi mkubwa kwamba, maji machafu ya nyuklia ya Japan yatasababisha upungufu wa chumi. Kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia cha Korea Kusini Lee Jae-myung, alitaja mpango huo wa Japan ni “kitendo cha ugaidi wa mionzi”, na kusisitiza kwamba asilimia 85 ya Wakorea Kusini wanapinga Japani kufanya hivyo.

Mpango wa Japan pia umepingwa vikali na nchi za visiwa vya Pasifiki. Katibu Mkuu wa Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki Henry Puna anaamini kwamba mpango huo wa Japana “utafungua sanduku la Pandora”, na haipaswi kusubiri miongo kadhaa kuelewa athari za mpango huo kwa Pasifiki. Kulingana na takwimu, nusu ya samaki aina ya Tuna duniani wanatoka katika nchi za visiwa vya Pasifiki, hivyo kitendo cha kumwaga maji taka ya nyuklia kinaweza kuwa na athari mbaya kwa uvuvi ambao unategemewa sana kwa uchumi wa nchi hizo. Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Menasi Sogavare ameeleza kushtushwa na Japani kwa kumwaga maji taka ya  nyuklia baharini, akisema iwapo maji hayo ni salama, basi yanapaswa kuhifadhiwa nchini Japan. Amesisitiza kuwa kitendo hicho ni pigo kubwa kwa uaminifu kati ya nchi duniani.

Kumwaga maji taka ya nyuklia baharini sio chaguo pekee kwa Japan. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ilikuwa na mipango mingine, ikiwemo kuweka matangi zaidi ya kuhifadhi maji hayo, kuanzisha maeneo mengine ya kuhifadhi maji hayo, na kuingiza maji hayo ardhini. Lakini ikilinganishwa njia nyingine, gharama za kutupa maji hayo baharini moja kwa moja ni ndogo zaidi. Japan, ikiwa nchi ya tatu kwa uchumi duniani, kitendo hiki ni cha kibinafsi na kutowajibika.