Wanasayansi wa Afrika na China waahidi ushirikiano katika kuendeleza ajenda endelevu
2023-09-28 23:18:10| cri

Wanasayansi kutoka China na nchi za Afrika wameahidi ushirikiano zaidi ili kufikia baadhi ya malengo ya Pendekezo la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ (BRI) ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula na afya ya mfumo wa ikolojia.

Katika maazimio yao yaliyopitishwa mwishoni mwa kongamano lililofanyika Nairobi nchini Kenya, wanasayansi wamesisitiza kuwa ushirikiano katika maeneo muhimu kama vile utafiti, uhamisho wa teknolojia na uboreshaji wa ujuzi utakuwa muhimu katika kubadilisha uchumi na kufufua uhifadhi wa makazi.

Wanasayansi karibu 100 wa China na Afrika walihudhuria kongamano hilo kuanzia tarehe 25 hadi 27 mwezi huu, lililoitwa "Ushirikiano wa Kusini-Kusini: Ushirikiano wa Sayansi na Teknolojia kati ya China na Afrika na Ubunifu kwa Manufaa ya Kijamii na Kiuchumi."

Washiriki wa kongamano hilo kutoka serikalini na taasisi za utafiti za Umoja wa Afrika na China walijadili kuimarisha ushirikiano katika maeneo matatu muhimu yakiwemo mabadiliko ya mifumo ya chakula, uhifadhi wa viumbe anuai na usimamizi wa maji.