China na Afrika zatangaza kwa pamoja pendekezo la kuhimiza maendeleo barani Afrika
2023-09-28 08:57:55| CRI

China na Afrika zimetangaza kwa pamoja pendekezo la “Kuimarisha uongozi wa China na Afrika katika Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia, na Kukuza Maendeleo Endelevu Barani Afrika”.

Pendekezo hilo limetambuliwa kwa pamoja na wanasayansi zaidi ya 100 kutoka China na Afrika, ambao wataanzisha kwa pamoja “Mpango wa Utekelezaji wa Ulinzi na Maendeleo ya Chakula, Maji, na Mazingira wa Afrika”, na utaratibu wa ushirikiano na kubadilishana wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na kati ya taasisi za sayansi na elimu za China, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika na mashirika ya kimataifa.

Pendekezo hilo limeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika, Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika na Chuo cha Sayansi cha China, pamoja na Mfuko wa Teknolojia ya Kilimo wa Afrika, Mamlaka ya Taifa ya Uvumbuzi ya Kenya, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta nchini Kenya, Chuo cha Sayansi ya Kilimo cha China na Kituo cha Uvumbuzi na Ushirikiano kati ya China na Afrika.