Rais wa China asisitiza nchi hiyo itashiriki kikamilifu katika mageuzi ya WTO
2023-09-28 20:26:22| CRI

Rais wa China, Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesisitiza kuwa China itashiriki kikamilifu katika mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kuongeza uwezo wa kufungua mlango katika kiwango cha juu.

Rais Xi amesema hayo alipohutubia Mkutano wa Nane kuhusu Mageuzi ya Kanuni na Mageuzi ya WTO ulioandaliwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa WTO ni nguzo muhimu ya utaratibu wa pande nyingi, na jukwaa muhimu la usimamizi wa uchumi wa kimataifa, na kwamba mageuzi ya Shirika hilo ni maoni ya pamoja ya watu, pia ni hatua inayoendana na wakati. Pia amesisitiza kuwa ni muhimu kuelewa kwa kina umuhimu na uharaka wa kushiriki katika mageuzi ya Shirika hilo kwa kuratibu hali ya ndani na ya kimataifa, maendeleo na usalama, kushiriki kwa pande zote katika mageuzi ya shirika hilo na marekebisho ya kanuni za uchumi na biashara duniani, na kuhimiza mageuzi ya kina na maendeleo ya hali ya juu kwa kufungua mlango katika kiwango cha juu.