Ubalozi wa China nchini Kenya waadhimisha miaka 74 ya Jamhuri ya watu wa China
2023-09-28 09:00:07| CRI

Ubalozi wa China nchini Kenya umefanya tafrija ya maadhimisho ya miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Tafrija hii imehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Kenya, mabalozi na wageni wengine wamealikwa.

Akiongea kwenye tafrija hiyo, Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhou Pingjian amesema China inauchukulia uhusiano kati ya China na Kenya kwa jicho la kimkakati, ikiongozwa udhati, matokeo halisi, undugu na nia njema, katika kuimarisha umoja na mashirikiano.

Waziri mwandamizi wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi amesema kwenye tafrija hiyo kuwa Kenya inaishukuru China kwa mchango wake kwenye maendeleo ya Kenya, na kupongeza ushirikiano kati ya China na Kenya chini ya kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.