Rais wa Tanzania aeleza kufurahia nchi yake kuandaa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda
2023-09-28 08:56:56| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameelezea furaha yake baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuzipa zabuni ya pamoja Tanzania, Kenya na Uganda ya haki ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Rais Samia aliandika kwenye mtandao wa kijamii kufurahia Kenya, Uganda na Tanzania kupata fursa ya kuandaa AFCON 2027 kwa pamoja.

Ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha usimamizi wa maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa viwanja vya michezo katika mikoa ya Dodoma na Arusha.