Mmoja auawa na 11 wajeruhiwa katika ajali ya mlipuko wa guruneti la roketi katika mashariki mwa DRC
2023-09-29 08:43:46| CRI

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC amesema, mtu mmoja ameuawa na wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya mlipuko wa guruneti la roketi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi katika mkoa huo Guillaume Kaiko Ndjike, mlipuko huu umetokea saa kumi mchana wakati guruneti la kurushwa kwa roketi RPG-7 lililokuwa limeshikwa na askari katika gari la kijeshi lilifyatuka kwa bahati mbaya kufuatia tukio la barabarani katika mji wa Goma.

Guruneti hilo la roketi liliangukia katika uwanja mmoja wa mji huo, na kuwajeruhi raia 11 wa kawaida, na askari mmoja alifariki kutokana na majeraha yaliyosababishwa na guruneti hilo.