Rais Xi Jinping asema kujiamini kuna "thamani zaidi kuliko dhahabu" kwenye safari ya ufufuaji mkubwa wa taifa
2023-09-29 22:58:26| cri
Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito kwa taifa kuimarisha imani na kujitahidi kupigania umoja katika jitihada zisizo na ukomo za kuijenga China yenye nguvu na kufikia ufufuaji mkubwa wa taifaa.
Akiongea kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China  Rais Xi amesema nguvu ya China inatokana na umoja na kujiamini ambavyo vinathamani zaidi kuliko dhahabu. Rais Xi ameongeza kuwa siku zijazo ni nzuri na taifa linapaswa kuendelea kukabiliana na changamoto na kusonga mbele.
Waziri mkuu wa China Bw Li Qiang aliongoza sherehe hiyo, ambayo pia imehudhuriwa na maofsa waandamizi wa China ikiwa ni oamoja na Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng pamoja na wageni wapatao 800 wa China na wageni.
Rais Xi amekumbusha kuwa katika kipindi cha miaka 74 tangu kuanzishwa kwa China Mpya, China imetoka kwenye hali ya umaskini na kufikia ustawi wa wastani katika pande zote, na imeanza safari mpya ya kujenga taifa lenye nguvu na uendelezaji mkubwa wa taifa katika pande zote kwa njia ya China kuelekea mambo ya kisasa.