Vyuo vikuu vya China vyapanda juu zaidi kwenye viwango vya dunia
2023-09-29 22:13:28| cri

Vyuo vikuu vya China vimepanda daraja la juu zaidi katika orodha ya vyuo vikuu kama elimu ya juu.

Kwa mujibu wa Viwango vya Elimu ya Juu ya Vyuo Vikuu Duniani vinavyotolewa kila mwaka (Times Higher Education World University Rankings) ambavyo vilichapishwa Jumatano, vyuo vikuu viwili vya China viliingia kwenye 15 bora kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 20 ya orodha hiyo.

Chuo Kikuu cha Tsinghua cha China kimeshika nafasi ya 12 kwenye orodha hiyo, na kupanda nafasi nne tangu mwaka jana, wakati Chuo Kikuu cha Peking kimepanda kutoka nafasi ya 17 hadi 14.

Kwa ujumla, China ina vyuo vikuu saba kati ya 100 bora, ikilinganishwa na vyuo vikuu viwili mwaka 2018, wakati idadi ya taasisi za China katika orodha ya 400 bora ikiongezeka mara mbili kutoka 15 mwaka 2021 hadi 30 mwaka huu.