EAC yahimizwa kutumia teknolojia mpya kukabiliana na magonjwa yanayoibuka
2023-09-29 08:46:35| CRI


 

Maofisa wandamizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutumia teknolojia mpya, ili kukabiliana na magonjwa yanayoibuka.

Maofisa hao wametoa wito huo kwenye Kongamano la 9 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika Jumatano huko Kigali, nchini Rwanda.

Waziri wa Afya wa Rwanda Bw. Sabin Nsanzimana amesema, teknolojia za kidijitali zitawezesha nchi wanachama wa EAC kutumia ipasavyo wafanyakazi na rasilimali zao chache, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa raia wao.