Peng Liyuan ahudhuria sherehe za tuzo za UNESCO kwa elimu ya wasichana na wanawake
2023-09-29 10:45:10| CRI

Mke wa Rais Xi Jinping wa China, Peng Liyuan na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Audrey Azoulay, Alhamisi walihudhuria hafla ya utoaji Tuzo za UNESCO za Elimu ya Wasichana na Wanawake za 2023 hapa mjini Beijing.

Peng, ambaye pia mjumbe maalum wa UNESCO kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya wasichana na wanawake, na Azoulay kwanza walitoa tuzo kwa wawakilishi walioshinda tuzo wa Mfuko wa Watoto na Vijana wa China (CCTF) na Muungano wa Pakistani wa Elimu ya Wasichana (PAGE).

Akitoa hotuba, Mama Peng alisema ushirikiano wa karibu wa China na UNESCO, hasa uanzishwaji wa tuzo ya elimu ya wasichana na wanawake umekuwa mfano, umetoa uzoefu wa thamani na kubeba jukumu la kupigiwa mfano katika maendeleo ya elimu ya wasichana na wanawake duniani kote.

Akibainisha kuwa elimu ya wasichana na wanawake inakabiliwa na hali, mahitaji na changamoto mpya katika ulimwengu wa leo, Mama Peng alitoa wito kwa pande zote kuongeza zaidi michango na uungaji mkono wao, kuendeleza kikamilifu elimu za afya, dijitali na sayansi kwa wanawake, na kuwasaidia wanawake zaidi kuboresha afya zao pamoja na kuimarisha uwezo wao wa kuvumbua na kuanzisha biashara.