Zambia kuhamasisha wenyeji kuhusu kufanya mwaka 2024 kuwa mwaka wa utamaduni na utalii wa China na Zambia
2023-09-29 08:35:51| CRI

Zambia inapanga kuhimiza uhamasishaji wa makubaliano kati ya China na Zambia kuufanya mwaka 2024 kuwa Mwaka wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Zambia, ili kuwawezesha wenyeji kushiriki katika kuhimiza sekta ya utalii na wenzao wa China.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii ya Zambia Bwana Evans Muhanga, amesema serikali kupitia wizara hiyo itapanga shughuli za kitamaduni katika maeneo ya utalii nchini kote, na kuangalia ushiriki wa wazambia ili kuimarisha mpango wa mabadilishano ya kiutamaduni na China.

Bwana Muhanga amesema mwaka wa Utamaduni na Utalii unakuja wakati Zambia inaimarisha ushirikiano wake na China kwa manufaa ya pande zote.

Pia amesema watalii kutoka China wanasafiri kwa makundi hali inayoihitaji sekta ya utalii kujiandaa kupokea idadi kubwa ya wageni kutoka China.