Wanafunzi wa Kenya washerehekea Sikukuu ya Mwezi ya China huku uhusiano kati ya China na Kenya ukiimarika
2023-09-29 08:36:28| CRI

Wanafunzi wa taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi, wamesherehekea Sikukuu ya Mwezi ya China (Mid-Autumn Festival), ili kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya China na Kenya.

Sherehe hiyo imewaleta pamoja zaidi ya watu 50, ikiwa inahusisha shughuli za muziki wa jadi wa China, ngoma, ngonjera, mashairi na pamoja na utayarishaji wa keki za mwezi na taa.

Mkurugenzi wa China wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi Wang Shangxue, amesema sikukuu hiyo husherehekewa nchini China kila mwezi unapokuwa mpevu, na familia hujumuika na kula keki za mwezi.