Kenya yatoa wito wa kubuniwa mfumo wa kifedha wenye uvumbuzi ili kuhimiza ukuaji wa kijani
2023-09-29 08:25:47| CRI

Kenya imetoa wito wa kubuniwa mfumo wa kifedha wenye uvumbuzi kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ili kupiga jeki ukuaji wa kijani.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Kenya Bw. Njuguna Ndung’u amesema mfumo mpya ya kifedha utaisaidia Afrika kupata fedha kwa ajili ya mipango yao ya kijani.

Waziri huyo amesema mfumo huo mpya unapaswa kushirikisha sekta binafsi na kuiruhusu kuchangia isiyozidi asilimia 26 ya fedha za tabianchi, ikiwa ni tofauti na mfumo uliopo ambao asilimia kubwa ya fedha zinatoka kwenye sekta ya umma.