Xi asema imani ni muhimu zaidi kuliko dhahabu kuelekea ustawishaji wa taifa
2023-09-29 10:44:23| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa taifa zima kuwa na imani thabiti na kujitahidi kwa pamoja bila ya kulegalega katika kujenga China yenye nguvu na kutimiza ustawishaji wa taifa.

Rais Xi, ambye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesema hayo katika tafrija kubwa iliyofanyika jana Alhamisi hapa Beijing kwa ajili ya kuadhimisha miaka 74 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Amesema nguvu zinazotokana na umoja na imani ni muhimu zaidi kuliko dhahabu.

Xi amebainisha kuwa mustakbali ni mzuri na taifa linapaswa kuendelea kushinda magumu na kusonga mbele.