Xi akutana na mkuu wa UNESCO
2023-09-29 10:43:33| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Audrey Azoulay mjini Beijing Alhamisi.

Rais Xi amesema China daima imekuwa ikiunga mkono kazi ya UNESCO, na pamoja na UNESCO, imetoa mchango chanya katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya kimataifa, akiongeza kuwa ushirikiano wa thamani kati ya China na UNESCO unapaswa kudumishwa.

Amesema China inapenda kufanya kazi kwa karibu zaidi na UNESCO ili kuendelea kuboresha uwezo na kiwango cha ulinzi wa urithi, na kukuza mawasiliano, kufunzana na kushirikiana kati ya staarabu mbalimbali, ili kuchangia amani ya dunia na kuwezesha ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake, Azoulay alisema serikali ya China siku zote imekuwa ikizingatia na kuunga mkono kikamilifu kazi ya UNESCO, na kwamba Tuzo za UNESCO za Elimu ya Wasichana na Wanawake zilizoanzishwa kwa msaada wa China zina jukumu muhimu katika kukuza elimu ya wasichana na wanawake kote duniani.