Ajali ya moto iliyotokea kwenye harusi nchini Iraq ilitokana na uzembe
2023-10-02 09:00:48| CRI

Mkurugenzi wa Kamati ya uchunguzi ya Iraq juu ya ajali ya moto Saad al-Dulaimi, Jumapili alisema ajali hiyo iliyotokea Jumanne iliyopita kwenye harusi huko kaskazini mwa Iraq haikuwa ya makusudi.

Akitangaza matokeo ya uchunguzi kwenye mkutano na wanahabari, mkurugenzi huyo alisema, ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 107 kwa ujumla, na wengine 82 kujeruhiwa, ilitokea baada ya kurusha fataki ndani ya ukumbi wa harusi wilayani al-Hamdaniya mkoani Nineveh, kaskazini mwa Iraq.

Saad al-Dulaimi alisema watu walijaa kupita kiasi ndani ya ukumbi huo, na vifaa vilivyoko kwenye paa la nyumba vinaweza kuungua kwa urahisi. Aidha amesema kamati imegundua kuwa hakukuwa na milango ya dharura mbali na milango midogo na michache ya huduma, na pia hakuna vifaa vya usalama.