Kenya yasajili ongezeko kubwa la mashambulizi ya mtandao wakati nchi hiyo ikikimbilia kuwa kitovu cha kidijitali barani Afrika
2023-10-03 08:45:54| CRI

Kenya imekumbwa na ongezeko la kasi la mashambulizi ya mtandaoni katika miaka sita iliyopita huku taifa hilo la Afrika Mashariki likikimbilia kuwa kitovu cha kidijitali barani Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu mjini Nairobi, Kenya, wakati nchi hiyo ikianza kuadhimisha Mwezi wa Oktoba wa Kutoa Ufahamu kuhusu Usalama wa Mtandao, ambao ni mpango wa kimataifa unaoleta pamoja washirika binafsi na wa umma ili kuwawezesha watumiaji wawe na ujuzi na maarifa ya kujilinda mtandaoni, kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya, Christopher Wambua, alisema nchi hiyo imesajili kesi milioni 860 za mashambulizi ya mtandao katika mwaka uliopita, ambapo nyingi zao zikilenga Miundombinu muhimu ya Habari (CII). Amebainisha kuwa kwa miaka sita iliyopita, mashambulizi ya mtandaoni yaliyolenga CII nchini humo yalifikia milioni 7.7 kila mwaka.

Hivyo amesema mwenendo huu unaifanya Kenya kuwa miongoni mwa nchi tatu zinazolengwa zaidi barani Afrika ikiwa nyuma ya Nigeria na Afrika Kusini.