Rais wa Tanzania amteua msemaji mkuu mpya wa serikali
2023-10-03 08:43:28| CRI

Ofisi ya rais imesema katika taarifa kwamba Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amemteua msemaji mkuu mpya wa serikali.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema kwamba Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari Maelezo ya Tanzania na msemaji mkuu wa serikali.

Kabla ya kuteuliwa kwake, Matinyi ambaye ni mwanahabari mbobezi na mwenye uzoefu mkubwa, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam. Matinyi amechukua nafasi ya Gerson Msigwa aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.