Jeshi la Sudan na RSF zanyoosheana vidole juu ya shambulizi la ubalozi wa Ethiopia
2023-10-04 09:07:27| CRI

Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) Jumanne zilishutumiana kushambulia kwa mizinga makao makuu ya ubalozi wa Ethiopia huko Khartoum.

SAF Jumanne ilitoa taarifa ikisema baada ya shambulizi kali la waasi wa RSF dhidi ya makao makuu ya ubalozi wa Ethiopia mjini Khartoum, wanamgambo walitoa taarifa wakitaka kushutumu SAF kwa kufanya shambulizi hilo.

Taarifa hiyo ya SAF ilisema tangu mapambano yatokee, SAF inaonyesha moyo mkunjufu katika kufuata sheria ya kibinadamu ya kimataifa na kuhakikisha usalama wa wale wanaolindwa, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya wajumbe wa diplomasia nchini humo.

Kwa upande wa RSF, ilishutumu SAF kushambulia kwa mizinga makao makuu ya ubalozi wa Ethiopia, na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo ya ubalozi katika eneo la Al Amarat mjini Khartoum.