Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania yatoa tahadhari kuhusu kukwama kwa shughuli za majini katika Maziwa Makuu
2023-10-04 08:45:44| CRI

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Jumanne ilitoa tahadhari juu ya kukwama kwa shughuli za majini zikiwemo usafiri na uvuvi, kutokana na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maziwa matatu.

Ikitoa utabiri wa hali ya hewa wa siku tano, mamlaka hiyo imesema kuwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia urefu wa mita mbili yanatarajiwa katika Maziwa Makuu matatu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa itakayoathirika kando ya bonde la Ziwa Victoria ni Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga, Geita, na Simiyu. Mikoa itakayoathirika kando ya Ziwa Tanganyika ni Kigoma, Rukwa, na Katavi na mikoa itakayoathirika kando ya Ziwa Nyasa ni Ruvuma, Mbeya, na Njombe.