Watu 21 wafariki dunia katika ajali ya basi iliyotokea Venice, nchini Italia
2023-10-04 08:48:20| CRI

Takriban watu 21 wamefariki dunia baada ya basi kuanguka kutoka kwenye daraja karibu na mji wa Venice nchini Italia, kisha kuwaka moto baada ya kuangukia kwenye reli.

Ripoti zilitofautiana sana kuhusu idadi ya waliojeruhiwa, ikikadiriwa kuwa ni kati ya watu 12 na 40. Miongoni mwao, wawili walikuwa mahututi na wengine wengi walijeruhiwa vibaya. Zaidi ya hayo, wengine "kadhaa" waliripotiwa kutojulikana waliopo. Idadi ya vifo inaweza kuongezeka ambapo waliojeruhiwa wanaendelea kutibiwa katika hospitali za eneo hilo.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ametoa rambirambi zake binafsi na kwa niaba ya serikali na kusema kwamba amefuatilia kwa karibu hali inavyoendelea.

Ikulu ya Quirinale mjini Roma imesema kwamba Rais wa Italia Sergio Mattarella alimpigia simu Meya wa Venice Luigi Brugnaro na kuelezea masikitiko yake juu ya ajali hiyo.