Heshima kwa wazazi ama wazee, ni tabia ama maadili yaliyopita mizizi hapa nchini China. Lakini maendeleo ya haraka ya kiuchumi, pamoja na kuongezeka kwa ubinafsi na kupungua kwa ukubwa wa familia, kumeondoa hadhi ya kijamii ya wazee nchini China. Mabadiliko haya yanaendana na ongezeko kubwa la idadi ya wazee. Nchi nyingi zinakabiliwa na ongezeko la idadi ya wazee, lakini China sasa ni nchi ambayo ina idadi kubwa zaidi ya wazee duniani.
Mwaka 2019, watu milioni 254 nchini China walikuwa na umri wa miaka 60 au zaidi. Na inakadiriwa kuwa kuufikia 2040, idadi hii itaongezeka hadi milioni 402, na kufanya karibu 28% ya idadi ya wazee. Mabadiliko haya yana madhara makubwa kwa afya ya akili kwa waze wa vijijini, ambayo inasababisha upweke wa wazee hawa, hasa pale watoto wao wanapoondoka nyumbani na kwenda mijini kutafuta kazi za vibarua. Je njia gani zinazotumika ili kuwapa faraja wazee hawa wa vijijini na kufanya wawe na maisha mazuri ya afya? Leo katika ukumbi wa wanawake tutaangalia namna wanawake wanavyojitolea kusaidia wazee hawa wa vijiji na kubwa tutakuwa naye mama Chen akitufafanulia zaidi.