WTO yapunguza makadirio ya ongezeko la biashara kwa mwaka 2023 hadi asilimia 0.8
2023-10-06 09:23:59| CRI

Shirika la Biashara Duniani (WTO) lilisema thamani ya biashara ya bidhaa ya dunia inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 0.8 mwaka huu, ikiwa chini ya nusu ya ongezeko la makadirio ya mwezi Aprili ya asilimia 1.7.

Kwa mujibu wa makadirio mapya ya biashara yaliyotolewa Alhamisi na WTO, wachumi wa WTO wamepunguza makadirio hayo kutokana na kushuka kwa thamani ya biashara ya bidhaa kulikoanzia katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2022.

WTO ilibainisha kuwa makadirio ya ongezeko la biashara ya bidhaa ya dunia ya mwaka 2024 ya asilimia 3.3, hayajabadilika na yale makadirio yaliyotolewa awali.