China yatoa salamu za rambirambi kuomboleza vifo vya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan
2023-10-08 20:41:24| CRI

China imetoa salamu za dhati za kuomboleza vifo vya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea katika Jimbo la Herat, Afghanistan, na kutoa rambirambi kwa familia za waathirika.  

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema hayo wakati ilipojibu maswali kuhusu tetemeko hilo lililotokea nchini Afghanistan. Pia imesema inaamini kuwa watu wa Afghanistan wataweza kushinda athari zinazoletwa na janga hilo na kujenga upya mapema nchi yao, na kwamba China itatoa msaada kadiri iwezavyo kutokana na mahitaji ya Afghanistan.