Si uhaba unaosababisha manung’uniko, bali ni mgawanyo usio na usawa; si umaskini unaosababisha manung’uniko, bali ni kutokuwepo kwa kuridhika
2023-10-08 20:39:26| CRI

Msingi wa dhana ya kuchangia ni kuzingatia itikadi ya maendeleo inayozingatia watu, inayoonyesha utambuzi wa taratibu wa ustawi wa pamoja. Ustawi wa pamoja ni lengo la msingi la Umaksi na limekuwa wazo kuu la watu wa China tangu nyakati za kale. Confucius alisema, "Si uhaba unaosababisha manung’uniko, bali ni mgawanyo usio na usawa; si umaskini unaosababisha manung’uniko, bali ni kutokuwepo kwa kuridhika." Mencius alisema, "Ninapokuwa na wazazi wenye umri mkubwa, nitawatendea huku nisisahau wazazi wa wengine wenye umri mkubwa. Ninapokuwa na watoto, nitawatendea huku nisisahau watoto wa wengine." "Kitabu cha Maadili – Maadili na vitendo vyake " kinaelezea vizuri kuhusu hali ya "jamii yenye maisha bora" na jamii ya "mapatano makubwa".