Takwimu za ukuaji uchumi wa china zinaisuta magharibi
2023-10-08 10:45:00| cri

Wakati baadhi ya watu katika nchi za Magharibi kwa mara nyingine tena wanaposema maneno mabaya kuhusu uchumi wa China, wachunguzi wengi wa kimataifa wanasema vinginevyo. Kwa kuona hali nzuri ya kuimarika kwa uchumi wa nchi ya China, wameeleza kuwa uchumi wa China ni thabiti, wenye nguvu na uko tayari kupata mwelekeo wa kupanda kwa ujumla.

Uchumi wa China umeendelea kuimarika kwa njia ya ujumla ya kuanza kurejea kukua kwa nguvu.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, Pato la Taifa la China lilirekodi ukuaji wa asilimia 5.5, ambao ni wa kasi zaidi kuliko asilimia 3 ya mwaka jana, na kasi zaidi kati ya nchi zenye uchumi mkubwa. Shirika la Fedha la Kimataifa lilikadiria kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2 mwaka huu, na kuchangia theluthi moja ya ukuaji wa dunia.

"Dalili zote zinaonyesha ukuaji mzuri," Khairy Tourk, profesa wa uchumi katika Taasisi ya Teknolojia ya Illinois huko Chicago, Marekani ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kwa kuchochewa na viwanda na sekta zinazoibuka zenye ushindani, uchumi wa China unabadilika kutoka ukuaji wa kasi ya juu hadi ukuaji wa kiwango cha juu. Hii inafanya uchumi kuwa endelevu zaidi.

Miezi saba ya kwanza ya mwaka huu ilishuhudia uwekezaji wa China katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu ukipanda kwa asilimia 11.5 kuliko mwaka jana, hasa kwa kasi zaidi kuliko ukuaji wa uwekezaji wake kwa ujumla. Mwezi Julai, pato la seli za jua na bidhaa za magari yanayotumia nishati liliongezeka kwa asilimia 65.1 na asilimia 24.9 mtawalia.

"Kwa kweli sikubaliani na dhana kwamba uchumi wa China uko katika matatizo makubwa ya kimfumo," Chris Torrens, Naibu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Uingereza nchini China, amesema hivi majuzi katika mahojiano na Televisheni ya Bloomberg.

Badala yake, ukuaji wake unaenda katika mwelekeo sahihi kadiri matumizi ya wanunuzi bidhaa yanavyoongezeka, amesema.

"Marafiki zaidi wa Marekani wamegundua kwamba dhana kuhusu China inaweza kuporomoka kiuchumi ... ni ndoto kabisa," Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng ameandika kwenye makala yake iliyochapishwa hivi karibuni na Gazeti la The Washington Post.