Mwanariadha wa Kenya aweka rekodi ya mbio za wanaume za Chicago
2023-10-09 08:30:04| CRI

Mwanariadha wa Kenya, Kelvin Kiptum amekuwa mwanaume wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa kutumia saa 2 na sekundi 35, na kuweka rekodi mpya ya dunia katika Mbio za Marathon za Chicago zilizofanyika jana jumapili.

Kiptum alivunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha mwenzake wa Kenya, Eliud Kipchoge katika mbio za mwaka jana za Berlin.

Hii ni mara ya tatu kwa wanaume kuweka rekodi katika mbio za Marathon za Chicago, ambapo rekodi ya kwanza iliwekwa na mkimbiaji Khalid Khannouchi wa Morocco mwaka 1999.