Tanzania ina matarajio makubwa na vijana katika harakati za kuhifadhi mazingira
2023-10-09 10:28:47| cri

Serikali ya Tanzania imesema ina matarajio makubwa na vijana katika utekelezaji wa mipango yake ya uhifadhi wake wa mazingira. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Bw. Danstan Kitandula amesema serikali inaweka wazi milango yake kwa vijana ambao wana ubunifu wa uhifadhi wa mazingira.

Amesema milango iko wazi kwa vijana wanaotaka kutekeleza miradi inayolenga kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na mipango ya upandaji miti, na kuwa serikali iko tayari kuwaunga mkono.

Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, pia amesema serikali inaendelea na mipango kadhaa katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.